Numbers 24:3-8

3 anaye akatoa ujumbe wake: “Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,
ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;

4 bujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,
ambaye huona maono kutoka kwa Mwenyezi,
Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania (pia 24:16).

ambaye huanguka kifudifudi, na ambaye macho yake yamefunguka:


5 d“Tazama jinsi yalivyo mazuri mahema yako, ee Yakobo,
maskani yako, ee Israeli!


6 e“Kama mabonde, yanaenea,
kama bustani kando ya mto,
kama miti ya udi iliyopandwa na Bwana,
kama mierezi kando ya maji.

7 fMaji yatatiririka kutoka ndoo zake;
mbegu yake itakuwa na maji tele.

“Mfalme wake atakuwa mkuu kuliko Mfalme Agagi;
ufalme wake utatukuka.


8 g“Mungu alimleta kutoka Misri;
yeye ana nguvu kama nyati.
Anayararua mataifa yaliyo adui zake,
na kuvunja mifupa yao vipande vipande;
huwachoma kwa mishale yake.
Copyright information for SwhKC